RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kutoa zawadi ya sh bilioni moja kwa timu ya taifa ya soka, Taifa Stars, iwapo itatwaa ubingwa wa michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024 inayopangwa kuanza Agosti 2 hadi 30 ikiandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda.








Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Julai 24, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi, amesema donge hilo ni motisha na kwamba ana imani Taifa Stars italipambania Taifa kwa jasho na damu na kupeperusha vyema bendera ya nchi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo













