ENEO la hifadhi ya Ngorongoro limeendelea kuwa kimbilio la wageni mashuhuri duniani ambapo siku ya leo, Meya wa Jiji la Dallas nchini Marekani, Mhe. Eric Johnson kwa mara ya kwanza ameshuhudia upekee wa vivutio vya utalii vilivyopo katika hifadhi hiyo.
Meya huyo aliyefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza amepokelewa na Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), Abdul-Razaq Badru na kuwaeleza kuwa eneo la hifadhi ya Ngorongoro lina utajiri wa vivutio vya utalii ikiwepo Kreta ya Ngorongoro, Wanyama wakubwa watano "Big Five", bonde la Olduvai lenye gunduzi mbalimbali za Zamadam, tambarare za Ndutu ambazo ni mazalia ya Nyumbu, mchanga unaohama, Nyayo za Laetoli zenye umri wa miaka milioni 3.7 iliyopita na vivutio vingine vingi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo
















