KAMISHNA Mkazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Zanzibar, Khatib Mwinyichande, amesema Tume hiyo ina nafasi ya kipekee na ya kikatiba katika kuhakikisha uchaguzi mkuu nchini unakuwa huru, haki na unaozingatia misingi ya utawala bora. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), kwenye banda la Tume hiyo, Mwinyichande alibainisha kuwa jukumu kubwa la Tume ni kulinda na kuhifadhi haki za binadamu pamoja na misingi ya utawala bora, jambo linaloifanya kuwa na nafasi ya moja kwa moja katika mchakato wa uchaguzi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo