Maji yaleta maisha mapya Simiyu

SIMIYU-Maisha ya wananchi wa Simiyu sasa yamebadilika. Mabadiliko haya sio miujuza au ndoto bali ni mwititio wa Serikali katika kuwasikiliza wananchi na kubadili maisha yao. 

Ile hali ya manadiliko ya tabia nchi inayoleta adha kwa viumbe mbalimbali duniani, ikiwamo wanadamu na mazingira imepata jibu. Ni mradi wa maji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi wa Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi Simiyu. Chanzo cha mradi huu ni ziwa Victoria. Thamani ya mradi ni Shilingi bilioni 440 na kwa awamu ya kwanza wanufaika watakuwa miji ya Lamadi na Nyashimo pamoja na Busega, Itilima, Bariadi, Lagangabilili na vijiji 103.

Utekelezaji wa mradi huu ni matokeo ya diplomasia nzuri ya Serikali na wadau wa maendeleo ambao wametoa sapoti kubwa katika kuanza kutekelezwa kwa mradi huu wa kimakakati ambao sio tu utawanufaisha wananchi kwa majisafi bali pia katika shughuli zao za kila siku ikiwamo kilimo.

Tunaweza kusema, jitihada hii ya serikali imeleta mwanga mpya wa maendeleo kwa wakazi wa Simiyu na wananchi wa Tanzania kwa ujumla.

Mapema tarehe 19 Juni, 2025 ni alama katika historia, ni siku ambayo haitosahaulika kwa wote wakiwemo wenyeji wa mkoani Simiyu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi wa Simiyu.

Mradi huu thamani yake ni takriban Shilingi bilioni 440. Thamani hii ni matokeo ya diplomasia nzuri na wadau wa maendeleo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambayo ni janga la kidunia, sio Tanzania pekee.

Wadau wa maendeleo waliotoa sapoti katika kufanikisha hatua hii ni pamoja na Mfuko wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (GCF) na Serikali ka Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo ya KfW.

Pamoja na yote, nao wananchi wa Simiyu wamejitoa katika kufanikisha kazi hii.

GCF ni moja ya taasisi kubwa kabisa Duniani inayojikita katika suala la mazingira na uwezeshaji wake. Kwa Simiyu imetoa kiasi cha Euro Milioni 102.7.

Fedha hii moja kwa moja imeunga mkono jitahada kubwa inayofanywa na Serikali sio tu kuhusumia wananchi, bali pia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, na kuleta maendeleo kwa wananchi.

Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi umeleta msukumo mkubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika nchi za ulimwengu wa tatu kwa kuwatumia wataalamu wa ndani na uwekezaji nafuu wa kitaalamu katika mabadiliko ya tabianchi.

Wadau wa maendeleo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Simiyu ni nchi ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya (KfW) ambapo imetoa kiasi cha Euro Milioni 26.1.

Hatua hii inaonesha uhusiano mzuri na wa muda mrefu na wadau haw awa maendeleo na nchi ya Tanzania.

Kufanikisha jambo hili kwa wananchi Serikali ya Tanzania nayo imewashika mono wananchi kwa kiasi cha Euro 40.7 ambayo inatoka katika vyanzo vyake vya ndani.

Pamoja na hilo wananchi wa Simiyu nayo katika kuhakikisha kila jambo linaenda sawa wamemewezesha kwa mchango wa dhati ambao thamani yake ni Euro Milioni 1.5. Hii ni picha halisi kuwa wananchi nao hawako nyumba katika mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa uchache mkoa wa Simiyu tunaweza kusema bado ni mpya ukilinganisha na mingine, mkoa ulianzishwa mwaka 2012. Jiografia yake ni moja ya maeneo yanayokabiliwa na athari za mabadiliko ya tabianchi, kama maeneo mengine Duniani yanavyokumbana na hali hiyo, athari hizo ni pamoja na kuongezeka kwa joto, majira ya mvua yasokuwa na uhakika na ya kutatanisha, pamoja na mafuriko.

Mabadiliko haya yameharibu vyanzo vya maji, kuweka ukakasi katika uendelezaji wa shughuli za kilimo, kuzorotesha huduma za umma ikiwamo mahudhurio ya shule kwa watoto na afya.

Hivyo, mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Simiyu unakuwa ni tiba ya athari zote hizi kwa wananchi, hivyo kuwainua katika siku mpya kabisa kwa kazi na maendeleo yao.

Kupitia mradi huu, wilaya tano za mkoa wa Simiyu zinaenda kunufaika na huduma yam aji ya uhakika kutoka ziwa Victoria.

Wakazi wa Busega, Bariadi, Itilima, Maswan na Meatu maisha yao yanaenda kubadilika kabisa, yaliyopita itakuwa ni historia.

Kwa ujumla zaidi ya wananchi 450 wanaenda kufaidika na mradi huu kuanzia majumbani hadi katika madneo ya umma ya huduma ikiwamo shule na vituo vya afya bila kusahau huduma za kilimo. Mradi utazalisha kiasi cha maji lita Milioni 70 kiasi ambacho ni zaidi ya mahitaji ya wananchi.

Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2025 ikiwa ni hatua ya awamu ya kwanza. Maendeleo ambayo yamefanyika ni hakika Serikali imenuia kufanikisha kazi hii ambayo inawahusu moja kwa moja wananchi wake.

Kazi ya kulaza bomba kwa umbali wa kilomita 460 inaendelea na ujenzi wa mfumo wa kisasa wa kutibu maji yatakayofikishwa kwa wananchi. Vijiji pembeni ya bomba kuu kwa umbali wa kilomita 24 vitapata huduma ya majisafi.

Mradi huu ni moja ya mfano hai Duniani kote, kwa namna serikali ya Tanzania inavyowapigania wananchi na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Ielweke kwa mujibu wa tafiti za wanazuoni wabobezi katika masuala ya mazingira, mabadiliko haya yanatokea katika nchi zilizopoiga hatua kubwa kwa viwanda na zile za ulimwengu wa tatu. Mabadiliko ya tabianchi hayachagui.

Mradi huu unagusa maeneo anuwai katika jamii yoyote, kuanzia mazingira hadi maisha ya kila siku.

Rais Dkt. Samia akiweka jiwe la msingi alitumia fursa hiyo kutoa shukran za wananchi wa Tanzania kwa mradi huo muhimu katika maisha ya kila siku.

Aliainisha kuwa hiyo ni hatua ya kufikia lengo la Serikali la huduma ya maji kwa wananchi kwa asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mjini.

Ni wazi kuwa wananchi wanatakiwa kushirikiana n wataalam kulinda na kutunza mradi huu ambao umelenga kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) limeainisha kupitia wataalam wake kuhusu pengo lililopo katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, ambapo kwa sasa athari za mabadiliko hayo zinaonekana katika kila pembe ya dunia na hakuna nchi ambayo ina kinga. Hivyo, mabadiliko yanaweza kuwa na athari mbaya zaidi katika nchi mbalimbali duniani.

Takwimu za kisasansi zinaonesha kuwa athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kiasi kikubwa zinatokana na uharibifu mkubwa wa mazingira, na tayari athari zake zinaonekana katika maeneo mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Nchi zinazoendelea kihistoria zimekuwa zikichangia asilimia ndogo tu ya utoaji wa hewa zenye madhara zilizosababisha mabadiliko ya tabianchi, na 1% ya watu wanaoishi katika nchi tajiri zaidi duniani wanawajibika kwa zaidi ya mara mbili ya kiwango cha uzalishaji wa hewa chafu zinazozalishwa na asilimia 50 ya wakazi wa nchi masikini duniani leo.

Nchi masikini pia zinakabiliwa na athari zenye madhara za hali mbaya ya hewa kwasababu zinategemea zaidi mazingira asilia kwa ajili ya chakula na ajira, na hazina pesa za kutumia kuweza kukabiliana na adhari hizo.

Zaidi ya miaka 50 iliyopita, zaidi ya vifo viwili kati ya vitatu , vilivyotokana na hali mbaya ya hewa, ikiwa ni pamoja na ukame, moto katika misitu ambavyo vimekuwa vikitokea katika takriban idadi ya nchi 47 masikini zaidi duniani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news