Michuano ya CECAFA Beach Soccer 2025 yasogezwa mbele

MOMBASA-Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) litatangaza tarehe mpya za uzinduzi wa michuano ya CECAFA Beach Soccer 2025 hivi karibuni.
CECAFA imeahirisha michuano hiyo iliyokuwa imepangwa kufanyika Julai 16 hadi 20,2025 mjini Mombasa, Kenya.

“Michuano hiyo imeahirishwa kufuatia ombi kutoka kwa Serikali ya Kaunti ya Mombasa na mamlaka husika za serikali ya kitaifa,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA, Auka Gecheo.

CECAFA itatangaza tarehe mpya kuambatana na ratiba za kimkakati za Serikali ya Kaunti ya Mombasa na kufanya kazi kwa karibu na washirika wa ndani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news