DODOMA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameshiriki Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika Uwanja wa Mnara wa Mashujaa, uliopo Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma leo Julai 25,2025.

Maadhimisho hayo yameongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Viongozi mbalimbali wameshiriki katika maadhimisho hayo wakiwemo viongozi wa Serikali, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, pamoja na Viongozi wa Dini.
















