DODOMA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar na Kuwasili jijini Dodoma kushiriki uzinduzi wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ambayo itazinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete leo tarehe 17 Julai 2025.

