DODOMA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili Jijini Dodoma kushiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yatakayofanyika katika Uwanja wa Mnara wa Mashujaa uliopo Mji wa Serikali-Mtumba Dodoma, siku ya Ijumaa tarehe 25 Julai, 2025.



