Rais Dkt.Samia afungua Kanisa la Arise and Shine lililopo Kawe

DAR-Leo Julai 5,2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan ameungana na waumini na wananchi katika ufunguzi wa Kanisa la Arise and Shine lililopo Kawe jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Samia amesema,ujenzi wa nyumba za ibada ni maelekezo ya Mwenyezi Mungu kama yalivyoandikwa katika Kitabu cha Hagai 1:8.

Pia,amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zote za kidini, kwani wanatambua na kuthamini mchango wao katika maendeleo ya taifa letu,pamoja na kujenga jamii yenye maadili na hofu ya Mungu.
Vilevile,amewasihi viongozi wa dini kuendelea kutoa mahubiri yenye kudumisha amani, umoja na utulivu, hasa tunapoendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu.

Hema hilo ambalo linatajwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 15 linaongozwa na Mtume Boniface Mwamposa ambapo linatarajiwa kuhudumia waumini 50,000 kwa wakati mmoja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news