DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu amemteua Gilead John Teri kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA).
TISEZA ilianzishwa kufuatia kutungwa kwa Sheria ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi namba 6 ya Mwaka 2025, ambapo imeunganisha majukumu ya kilichokuwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA).
