DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Julai 8,2025 Ikulu jijini Dar Es Salaam amepokea Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Congo- Brazzaville,Mhe. Denis Sassou Nguesso uliowasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo,Mhe. Jean-Claude Gakosso.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo-Brazzaville, Mhe. Jean-Claude Gakosso, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Julai 8,2025 baada ya kiupokea Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Congo- Brazzaville,Mhe. Denis Sassou Nguesso uliowasilishwa kwake na waziri huyo.


