Tanzania na Oman zasisitiza umuhimu wa kusani makubaliano ya kazi na ajira



MUSCAT-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma M. Rajab amefanya mazungumzo na Waziri wa Kazi wa Oman, Prof. Mahad Said Ali Baawain, yalifanyika katika Ofisi za Wizara hiyo Julai 08, 2025.
Wawili hao pamoja na mambo mengine walijadiliana namna ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia ambao umedumu kwa muda mrefu kati ya Tanzania na Oman.

Balozi Fatma alieleza kuwa, moja ya eneo ambalo Tanzania na Oman zinashirikiana ni sekta ya kazi na ajira na kusisitiza ili uhusiano huo uendelee kunawiri na kuwa na manufaa kwa pande zote mbili, kuna umuhimu wa kuharakisha Rasimu ya Makubaliano ya Kazi na Ajira ili iweze kusainiwa hivi karibuni.
Balozi Fatma alisema Tanzania ni moja ya nchi zinazopeleka kiasi kikubwa cha wafanyakazi nchini Oman na ili iweze kuendelea kufaidika na soko la Ajira katika sekta mbalimbali, ni muhimu makubaliano hayo yakamilike na kusainiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news