Tuwalee vijana katika maadili na tudumishe amani-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa wito kwa wazazi, walezi, jamii na waumini wa dini ya Kiislamu kwa ujumla kuwalea vijana katika maadili mema, huku akisisitiza umuhimu wa kudumisha amani hasa tunapoelekea katika kipindi cha uchaguzi.Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 11 Julai 2025, mara baada ya kusali Sala ya Ijumaa, Masjid Lilah Kianga, Mkoa wa Mjini, Wilaya ya Magharibi ‘A’.

Katika salamu zake, Rais Dkt.Mwinyi amegusia maudhui ya hotuba ya Ijumaa iliyolenga malezi bora ya vijana na umuhimu wa kusali, akibainisha kuwa vijana wengi wamekuwa wakikosa mwelekeo sahihi na kujiingiza katika vitendo viovu kama vile dawa za kulevya, ujambazi na wizi, hali inayosababisha mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi ameshukuru uongozi wa msikiti wa Masjid Lilah kwa kumpa fursa ya kutoa salamu, akisisitiza kuwa viongozi wa dini wana nafasi muhimu katika kulea jamii kimaadili na kiroho.

Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa maendeleo, ibada na ustawi wa jamii haviwezi kupatikana bila kuwepo kwa amani ya kudumu. Kwa msingi huo, amehimiza viongozi wa dini na wa kisiasa kushirikiana kuhakikisha amani inaendelea kulindwa na kuenziwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news