Wananchi wamiminika banda la Ofisi ya Waziri Mkuu maonesho ya Sabasaba

DAR-Wananchi mbalimbali wameendelea kutembelea katika banda la Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na tsasisi zake ili kupata elimu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama SABASABA yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Aidha, wameonesha kuridhishwa na huduma zinazitolewa na ofisi hiyo pamoja na mambo mengine wamepata elimu kuhusu masuala ya vijana, ajira ulemavu na Uratibu wa Shughuli za Serikali.
Maonesho hayo kwa mwaka huu yana Kauli Mbiu inayosema “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa sabasaba, Fahari ya Tanzania” tarehe 03 Julai, 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news