Wataalamu wa BoT waendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mikopo salama Nyanda za Juu Kusini

IRINGA-Wataalamu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wanaendelea na kampeni maalum ya utoaji wa elimu kwa umma kuhusu mikopo salama pamoja na utaratibu wa kupata leseni ya utoaji wa huduma za kifedha.
Kampeni hiyo ilianza rasmi siku ya Jumatatu, Juni 30, 2025, na inafanyika katika mikoa ya Iringa na Njombe.

Inatarajiwa kukamilika Ijumaa, Julai 4, 2025, ikiwalenga wafanyabiashara, wajasiriamali na wananchi kwa ujumla.
Leo, Jumanne Julai 1, 2025, wataalamu walioko mkoani Iringa wametembelea masoko ya Mwamwindi na Lavela ambapo walizungumza moja kwa moja na wafanyabiashara.

Wakati huo huo, timu ya wataalamu walioko Njombe wameendesha mahojiano katika kituo cha redio cha Kings FM kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu masuala hayo.
Kampeni hii inatekelezwa kufuatia matokeo ya uchunguzi uliofanywa hivi karibuni na BoT kupitia ripoti maalumu iitwayo Kimangala Report, ambayo ilibaini kuwa wakazi wa mikoa hiyo ni miongoni mwa waathirika wa mikopo isiyo rafiki inayojulikana kama "mikopo umiza" au Kimangala.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news