WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Kampuni ya Minara Tanzania, ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo, Bw. Richard Cane, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuendeleza ushirikiano katika kukuza Sekta ya Mawasiliano nchini.











