Waziri Ulega akutana na mtoto mwenye kipaji cha ujenzi wa barabara na madaraja

DAR-Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amekutana na mtoto Ridhiwani Martin Asheri mwenye umri wa miaka 13 kutoka Kibaigwa mkoani Dodoma, mwenye kipaji cha ujenzi wa madaraja na barabara.
Waziri Ulega amekutana na mtoto huyo Julai 20, 2025 katika Ofisi ndogo za Wizara hiyo jijini Dar es salaam, na kufanya nae mazungumzo akiwa ameongozana na familia yake.

Baada ya mazungumzo hayo Waziri Ulega ameahidi kumsaidia kijana huyo kuhakikisha anatimiza ndoto zake za kuwa Mhandisi mkubwa hapo baadaye.

Waziri Ulega amesema, atakaa na Wizara ya Elimu kuona ni sehemu gani sahihi kijana huyo apelekwe ili kuweza kumsaidia kielimu hasa kwenye maswala ya ujenzi.

Pia,Waziri Ulega amemtembeza mtoto huyo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ili aweze kujionea kwa macho yale ambayo alikuwa anayatengeneza akiwa nyumbani kwao kwa kuyaona tu kwenye TV.

Miongoni mwa maeneo hayo ni Daraja la Kijazi lililopo Ubungo, Daraja la Tanzanite na kituo cha Treni ya Mwendokasi (SGR) Posta.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news