Askofu mstaafu Dkt.Martin Shao afariki

KILIMANJARO-Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini Dkt.Martin Shao amefariki dunia Agosti 25, 2025 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya kaskazini (KCMC) Mjini Moshi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Agosti 25, 2025 na Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Zebadiah Moshi imeeleza kuwa, Askofu huyo amefariki dunia asubuhi ya Jumatatu hospitalini hapo na kubainisha kuwa uongozi wa Dayosisi kwa kushirikiana na familia ya marehemu wanaendelea na maandalizi ya mazishi ambapo taratibu zitatangazwa baada ya kukamilika.

Dktt. Shao amehudumu kama Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini kuanzia mwaka 2004 hadi 2014 alipostaafu na nafasi hiyo kuchukuliwa na Dk Fredrick Shoo ambaye anaishikilia mpaka sasa.

Dkt. Shoo amesema, watamkumbuka marehemu Shao kwa hekima na busara zake katika kipindi chake cha utumishi na hata alipostaafu.

"Ni kweli baba yetu amefariki leo, alikuwa baba mwenye hekima nyingi, busara na moyo wa utumishi, amefanya mengi, tutamkumbuka kwa mengi katika Dayosisi yetu," amesema Dkt. Shoo akizungumzia msiba huo huku uongozi wa Dayosisi ukituma salamu za pole kwa familia ya marehemu, waumini wa KKKT na wote walioguswa na msiba huo mkubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news