BoT yatunukiwa tuzo ya Mshindi wa Kwanza kwa utawala bora na uwajibikaji

ARUSHA-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetunukiwa tuzo ya Mshindi wa Kwanza katika kundi la mashirika ya kibiashara na yasiyo ya kibiashara, ikiwa ni uthibitisho wa dhamira yake ya kuendeleza viwango vya juu vya utawala bora, uwazi na uwajibikaji wa taasisi.
Tuzo hiyo imetolewa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kukabidhiwa kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma iliyofanyika jijini Arusha tarehe 24 Agosti 2025.

Vigezo vilivyotumika katika utoaji wa tuzo hiyo vilijikita katika utekelezaji wa mapendekezo ya ukaguzi kwa kiwango cha juu, upatikanaji wa maoni chanya ya ukaguzi, uwazi katika kuchapisha taarifa za kifedha, pamoja na tathmini nzuri ya utendaji wa Bodi ya Wakurugenzi.
Mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za pamoja za menejimenti, wafanyakazi na viongozi wa Benki Kuu katika kutekeleza majukumu yake kwa weledi na kwa manufaa ya Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news