DAR-Leo Agosti 31,2025 jijini Dar es Salaam, Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimezindua rasmi kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025.
Katika uzinduzi huo, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupita Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalim amesema,iwapo Watanzania watawapa ridhaa ya kuongoza nchi wanatarajia kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo maboresho ya tasnia ya habari nchini.
Vilevile katika eneo la utumishi wa umma amesema, atahakikisha nidhamu kwa kila mtumishi na kuwaboreshea maslahi yao kwa kuanza na msharaha wa kima cha chini shilingi 800,000 baada ya makato ya kodi.
Mbali na maboresho katika sekta nyingine ikiwemo ya afya na huduma za afya, pia amesema Serikali yake itahakikisha inaongeza nguvu kwenye sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kuwezesha kuwa na uhakika wa chakula na mazao ya biashara kote nchini.





