ZANZIBAR-Wakati mwingine thamani ya kikao haipimwi kwa ukubwa wa meza au idadi kubwa ya watu, bali kwa mazungumzo yenye tija, hali inayoimarisha ukaribu na wazee na kufungua milango ya busara, heshima na mshikamano wa kweli.
Katika kampeni za mwaka 2020, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi alionesha dhamira ya kusikiliza kila kundi la wananchi akiheshimu mila na desturi zao.
Ziara zake zililenga kujenga umoja na kuendeleza mshikamano, kwa sasa si tu wazee wana mengi ya kusimulia kuhusu uongozi wake, bali pia makundi mengine yana mengi huku wakijivunia uongozi wenye neema tupu Zanzibar.
Katika picha hii, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi anaonekana akiwa pamoja na wazee maeneo ya Bweleo, Mkoa wa Mjini Magharibi, akizungumza nao na kushuhudia mchezo wa bao.
