Loji ya Kifahari ya Mapito Safari Camp yazinduliwa Serengeti kwa Ubia wa Delaware Investment na Marriot International

SERENGETI-Loji ya Kifahari ya Mapito Safari Camp itakayoendeshwa kwa ubia kati ya Kampuni ya Delaware Investment na kampuni kubwa duniani ya Marriot International imezinduliwa Agosti 29, 2025 katika eneo la Robanda, Serengeti nje kidogo ya hifadhi yenye mvuto duniani ya Serengeti.
Huu ni uwekezaji wa chapa mbili namba moja duniani, Serengeti ikiwa hifadhi namba moja Afrika na Dunia kwa ukubwa na mchanganyiko murua wa wanyama wengi na moja kwa tukio la wanyama wanaohama.

Kwa upande mwingine Marriot International, kampuni inayoongoza duniani kwa kumiliki au kusimamia hoteli na loji na kwa ujumla ikiwa namba moja duniani kwa kumiliki au kusimamia vyumba vingi vya kulala. Hii inaweza kuitwa “a meeting of two firsts.”
Hii inakuwa loji ya kwanza katika maeneo ya karibu ya Hifadhi kwa Marriot kujihusisha nayo hata hivyo haitakuwa ya mwisho hapa Tanzania.

Kutokana na sera nzuri na mvuto wa utalii nchini Tanzania tutarajie jingine kubwa: mwaka 2026 kampuni hiyo pia inatarajiwa kufungua hoteli ya kifahari ya vyumba zaidi ya 30 ya JW Marriot Serengeti Lodge ikiwemo vyumba vya kulala wageni wa hadhi ya juu kabisa (Presidential Suites) viwili inayoendelea kujengwa ndani ya Hifadhi ya Serengeti.
"Mapito Safari Camp, inaashiria tukio muhimu katika mkusanyiko wa kiotomatiki (Autograph Collection) tunapotambulisha uzoefu wa kwanza wa safari wa chapa hii katika mojawapo ya maeneo pori ya kuvutia zaidi duniani,"amesema Jerome Briet,Afisa Mtendaji Mkuu wa Maendeleo anayesimamia maendeleo kwa nchi za Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika kutoka Kampuni ya Marriott International.

Marriot imejenga,pia inasimamia kwa ubia au kibiashara zaidi ya maeneo 9,000 ya kulaza wageni iwe hoteli au loji katika nchi 144 na wakifanya kazi kwa muungano wa kibiashara na zaidi ya chapa 40 tofauti tofauti.

Huu ni mwendelezo wa sio tu hifadhi ambazo ni vituo muhimu vya utalii nchini bali Tanzania kwa ujumla wake kuendelea kupokea uwekezaji wa kampuni zenye majina makubwa katika utalii kufuatia filamu ya Royal Tour iliyomshirikisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akitangaza utalii na vivutio vingine nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news