Maelfu wamsindikiza Dkt.Biteko kuchukua fomu kugombea ubunge Jimbo la Bukombe

GEITA-Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukombe, Zedekiah Solomon Osan amemkabidhi fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Doto Mashaka Biteko leo Agosti 26, 2025 katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bukombe mkoani Geita.
Makabidhiano hayo ya fomu ni utekelezaji wa ratiba kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29,mwaka 2025. Aidha, maelfu ya wana CCM na wapenzi wa chama hicho wamemsindikiza mgombea kwa ajili ya kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa na Tume huru ya Uchaguzi.

Katika hali isiyo ya kawaida, zaidi ya wanama 1000 wamejotokeza kumdhamini Dkt. Biteko ikilinganishwa na mahitaji ya wadhamini 31 waliohitajika kisheria.
Akiwa katika Ofisi za Tume, amekabidhiwa fomu hizo na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Bukombe, Zedekiah Solomon Osano.

Akizungumza na wanaCCM katika viwanja Ofisi ya CCM Wilaya ya Bukombe, Dkt. Biteko amewataka wananchi kudumisha mshikamano na upendo miongoni mwao na kuwachagua viobgozi bora.
"Utakapofika wakati tuwachague viongozi tunaowapenda, nawaomba mmchague Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais, mnichague mimi kuwa mbunge na niwaaombe mniletee madiwani wa CCM tuendeleze kazi tuliyokwisha ianza.”
Awali, Katibu wa CCM, Wilaya Bukombe Leonard Mwakalukwa amesema,wana CCM zaidi ya 3,500 wamejitokeza kumsindikiza mgombea katika Ofisi za tume huru ya Uchaguzi kwa ajili ya kuchukua fomu.

Amesema,wadhamini 31 kutoka Kata zote 17 za Bukombe wamewawakilisha wenzao 969 waliojitokeza kumdhamini mgombea..

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news