MGOMBEA wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu amesema yeye na Mgombea Mwenza wa nafasi ya Makamu wa Rais, Devotha Minja wanaingia kwenye kinyang’anyiro cha urais wakiwa wasafi na hawana deni na mtu yeyote.

Mwalimu ameeleza hayo Agosti 12, 2025 baada ya kukabidhiwa Fomu ya uteuzi wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mstaafu Jacobs Mwambegele kwenye Ofisi za Makao Makuu ya tume hiyo zilizopo Njedengwa mkoani Dodoma.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo












