MGOMBEA urais wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Kyara ameahidi kuwa endapo chama hicho kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2025 kitahakikisha kinapunguza gharama za umeme ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa maisha.







Kyara akiwa amongozana na Mgombea Mwenza wa nafasi ya Makamu wa Rais, Satia Bebwa ametoa kauli hiyo Agosti 13, 2025 mjini Dodoma baada ya kukabidhiwa Fomu za Uteuzi wa nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele katika Ofisi za Makao Makuu ya tume hiyo zilizopo Njedengwa jijini humo.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo


















