SERIKALI imeendelea kuwekeza katika vifaatiba vya kutibu magonjwa mbalimbali nchini ikiwemo ya Figo ambapo hadi kufikia mwezi Agosti mwaka huu, 2025 idadi ya mashine za kuchuja damu 137 kutoka mashine 60 za awali zimenunuliwa na kusambazwa katika hospitali 15 kutoka hospitali 6 kupitia Bohari ya Dawa nchini (MSD) katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ameeleza hayo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo Agosti 15, 2025 mkoani Dodoma alipokuwa akielezea mafanikio ya Bohari ya Dawa (MSD) kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo



















