SERIKALI za Afrika ya Mashariki,l zimeombwa kuondoa vikwazo ambavyo vinaathiri biashara za mipakani za mazao ya Kilimo Ikololojia, hasa kwa wajasiriamali wadogo ili kuwezesha kukuza biashara hiyo.
Utafiti uliofanywa kuhusiana na biashara za kilimo ikolojia (Kilimo Hai) mipakani zimebaini, kuna changamoto kadhaa ikiwemo viwango vya ubora wa bidhaa,mifumo ya ulipaji kodi,vikwazo vya barabarani,udhibiti wa bidhaa zisizo na ubora na uelewa mdogo wa wajasiriamali katika masuala ya biashara ya mipakani.Akisoma mapendekezo ya kisera kutokana na warsha ya wadau kuhusu biashara ya mipakani kwa mazao ya bidhaa za kilimo kkolojia, Afisa wa Utetezi na Ushawishi wa Shirikisho la Wakulima Tanzania (SHIWAKUTA), Thomas Laizer amesema, wamekubaliana ni muhimu, kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kuondoa au kupunguza vikwazo visivyo vya kikodi (NTBs) ikiwemo mazuio yasiyo rasmi ya barabarani ambayo kwa kiasi kikubwa yanaathiri biashara za mipakani.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






















