MBUNGE wa Viti Maalum anayemaliza muda wake na Msanii, Khadija Taya (Keisha) ameshindwa kufurukuta katika kura za maoni kupitia Jumuiya ya wazazi Tanzania Bara yenye nafasi moja baada ya kupata kura 94 kati ya kura halali 708.
Katika kundi hilo lililokuwa na wagombea 18, Catherine Joachim alipata kura 567 kati ya kura halali 708. Kwa upande wa Zanzibar, Mbunge wa viti maalum, Najma Murtaza Giga ameongoza kundi hilo baada ya kupata kura 591 na kuwaacha mbali wapinzani wake watano.
Katika kundi la wabunge wa viti maalum kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi lenye nafasi mbili aliyeongoza ni Aza Januari Joseph aliyepata kura 350 kati ya kura halali 702 na Salama Abasi Juma aliyepata kura 330. Kundi hili lilikuwa na wagombea nane.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo













