WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe meiagiza Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) kwenda kuwakamata na kuwafungulia mashitaka wauzaji wa pembejeo bandia ikiwemo mbegu za kilimo kwa mujibu wa sheria.
Bashe ameeleza hayo Agosti 22, 2025 mkoani Dodoma wakati akizindua Bodi ya Wakurugenzi ya TOSCI ambapo ameitaka kwenda kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika kupambana na tatizo hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk. Lilian Shechambo ametaja vipaumbele mbalimbali ambavyo bodi hiyo itakwenda kuvitekeleza ikiwemo kuendelea kuimarisha shughuli za usajili wa watoa huduma za mbegu (Seed Dealers) kwa kutoa mafunzo, ukaguzi na miongozo.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo


















