Mifugo 148,172 katika Halmashauri ya Mji Handeni, mkoani Tanga, inatarajiwa kuchanjwa dhidi ya magonjwa ya kideri, sotoka na mapafu, kupitia kampeni ya kitaifa ya chanjo ya mifugo.
Akizindua kampeni hiyo Agosti 22, 2025 katika Kata ya Malezi, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Salum Nyamwese, amewahimiza wafugaji wote wa Halmashauri hiyo wajitokeze kishiriki zoezi hilo la kitaifa ili kukabiliana na magonjwa ya mifugo.







Kwa upande wake, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri hiyo, Aldegunda Matunda, amesema kati ya idadi hiyo ya mifugo; ng’ombe ni 38,006, mbuzi 25,356, kondoo 9,567 na kuku 75,243.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo







