WAZAZI wamehimizwa kuwatibu watoto wanaopata ugonjwa wa mafindofindo (tonsillitis) kuwaepusha na hatari ya kupata magonjwa ya valvu za moyo.
Hayo yamesemwa na Daktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Salehe Mwinchete wakati wa kambi maalumu ya siku nne ya upasuaji wa moyo iliyokuwa ikifanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Madaktari Africa la nchini Marekani.Dkt. Salehe alisema, tatizo la valvu za moyo kuziba uanza na maambukizi ya kooni yajulikanayo kama mafindofindo (tonslight), na homa za utotoni za mara kwa mara ambazo huleta maambukizi yanayoathiri koo na wadudu wake kwenda kuharibu milango ya moyo (Valvu za moyo).
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo




.jpg)



















