MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila amewataka wanasheria wa taasisi hiyo kuwadhibiti baadhi ya wagombea watakaobainika kutoa rushwa katika kipindi hichi cha uchaguzi kwa kufanya uchunguzi wa kina na wenye tija.
Chalamaila alitoa agizo hilo wakati akifungua mafunzo ya kuimarisha weledi wa taaluma ya sheria kwa wanasheria zaidi zaidi 300 wa taasisi hiyo kutoka mikoa yote nchini yaliofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Mjini Kibaha mkoani Pwani.
Alisema, majukumu makuu ya taasisi hiyo ni kutoa elimu ya rushwa kwa umma, kuzuia rushwa na kufanya uchunguzi na kwamba katika kipindi hichi cha uchaguzi ni wanasheria hao wanajukumu kubwa la kuchunguza vitendo vya rushwa na kudhibiti hatua itakayosaidia upatikanaji wa viongozi bora.
"Sasa tunaelekea katika kipindi cha kampeni ambacho kitachukua miezi miwili, ni wakati wenu kufanyakazi ili kuchunguza vitendo vya rushwa ni dhahiri kwamba viongozi ambao wanaopatikana kwa njia ya rushwa ni ngumu kuwa viongozi bora hataweza kutusaidia kusimamia miradi,"alisema.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






























