BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limetoa mafunzo kwa Maafisa wa Uthibiti Ubora, Wakuu wa Vyuo na Wakuu wa Idara kutoka vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi katika Kanda ya Mashariki, kwa lengo la kuongeza ufanisi katika usimamizi wa vyuo hivyo na kuhakikisha ubora wa mafunzo unaboreshwa ili kuzalisha wahitimu wenye sifa zinazohitajika katika soko la ajira.


Akizungumza Agosti 27, 2025 jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora kutoka NACTVET, Dkt. Jofrey Oleke, amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuboresha ubora wa elimu inayotolewa katika vyuo vinavyosimamiwa na NACTVET, hususan katika maeneo ya utoaji wa elimu na uandaaji wa mitaala.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo



























