MKOA wa Geita unatarajia kupokea Mwenge wa Uhuru Jumatatu ya Septemba 01, 2025 katika kijiji cha Rwezera ukitokea Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella ametoa taarifa hiyo Agosti 30, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
Shigella amesema kwa mwaka 2025 Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Geita unatarajia kupita na kukimbizwa katika jumla ya miradi 61 yenye thamani ya sh bilioni 164.4.
Amesema mwaka 2024 mwenge wa Uhuru ulikimbizwa ndani ya mkoa wa Geita na kuweza kufikia miradi 65 yenye jumla ya thamani ya Sh bilioni 32.2.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo













