MWONGOZO wa Kuanzisha na Kuendesha Shamba Darasa la Kilimo Biashara umezinduliwa rasmi Agosti 2, 2025 katika Kongamano la wadau wa kilimo lililofanyika sambamba na Maonesho ya Wakulima (Nanenane) katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli amesema mwongozo huo unaolenga kuwainua wakulima wa kawaida umezingatia vipengele mahususi ambavyo ni Uwezeshaji, Kilimo himilivu, Dhana ya biashara katika kilimo, Masuala ya usawa katika kilimo, kujikinga na magonjwa ya kuambukiza pamoja na uongezaji thamani katika mazao ya lishe,Aidha, Katibu Mkuu huyo amewataka wadau wote wa sekta ya kilimo kuutekeleza mwongozo huo ili kuongeza thamani ya fedha katika sekta hiyo.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo













