ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation(ZMBF), Mhe. Mama Mariam Mwinyi amewasili Pemba kwa ajili ya kufunga Kambi ya tano ya Afya Bora, Maisha Bora inayofanyika katika viwanja vya Hospitali ya Wilaya ya Vitongoji, Mkoa wa Kusini Pemba.
Katika uwanja wa ndege wa Pemba amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe.Rashid Hadid Rashid na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi na vyombo vya ulinzi na usalama.





