Mchengerwa ashinda kwa asilimia 99.19 Rufiji

NA ALLY ISSA

MGOMBEA wa Jimbo la Rufiji anayetetea jimbo lake Mohamed Mchengerwa ameibuka kidedea katika kinyang'anyiro cha kura za maoni kwa kuzoa asilimia 99.19 ya kura zote zilizopigwa.Akitangaza matokeo hayo Mkurugenzi wa Uchaguzi wa jimbo hilo Prudence Sempa. amesema Mchengerwa amepata kura 8, 465 kati ya kura 8 , 533 zilizopigwa sawa na asili 99.19

Aidha, Sempa amesema kura zote zilizopigwa zilikuwa 8, 534 ambapo idadi ya kura zilizoharibika ni asilimia 0.01 ya kura zote halali.
Wagombea wengine Salma Hamis ,Selemani Mhekela na Hamisa Kisoma waligawana asilimia iliyobaki.

Baada ya kutangaza matokeo hayo wagombea hao wamempongeza Mchengerwa na kuahidi kushirikiana na yeyote kati yao ambaye atachaguliwa na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) miongoni mwao kupeperusha bendera katika uchaguzi mkuu.
Naye Mchengerwa amewashukuru wajumbe kwa kumpa kura za kishindo huku akisema kuwa ana deni kubwa la kuwalipa endapo Chama chake CCM kitampitisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news