Mfumo wa Hazina ya Machapisho (Mof respository) ni nyenzo muhimu kwa wananchi na watafiti

PETER HAULE NA
SAIDINA MSANGI

MSIMAMIZI wa Kitengo cha Maktaba, Wizara ya Fedha, Bi. Pendo Kavalambi, amesema kuwa Mfumo wa Hazina ya Machapisho (Mof respository) umekuwa nyenzo muhimu kwa wananchi wakiwemo wanaofanya tafiti kuhusu masuala ya uchumi na fedha.
Msimamizi wa Kitengo cha Maktaba, Wizara ya Fedha, Bi. Pendo Kavalambi, akitoa elimu kwa, Bi. Mariam Mayunga, kuhusu Mfumo wa MoF Repository wenye taarifa za uchumi na Fedha tangu uhuru, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.

Amesema hayo jijini Dodoma wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.
Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo, akitoa elimu kuhusu akiba kwa mfanyabiashara wa mitumba wa jiji la Dodoma Bw. Sam Abdalah, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.

Bi. Kavalambi amesema kuwa,mfumo huo ambao unapatikana kirahisi kwa njia ya simu janja na vifaa vingine vya kielektroniki kama kompyuta unamuwezesha mtumiaji kupakua taarifa za hali ya uchumi, deni la Taifa, Sheria ya Fedha na Bajeti Kuu ya Serikali tangu uhuru.

Alisema machapisho hayo yanasaidia kuongeza ufahamu wa masuala ya uchumi na kuwasaidia vijana kufahamu juhudi zilizofanywa na Serikali katika kupiga hatua za maendeleo tangu kupatikana kwa uhuru. Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na TEHAMA,Wizara ya Fedha, Bw. Charles Maganga, akitoa elimu ya Mifumo ya Fedha kwa Bw. Leonard Maona, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.
Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Boniface Kilindimo, akitoa elimu kuhusu uhusiano wa Bajeti Kuu ya Serikali na Maendeleo ya Wananchi, kwa wakazi wa Dodoma walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.

Bi. Kavalambi alisema, kizazi cha sasa hakina taarifa ya kutosha kuhusu mwenendo wa uchumi tangu uhuru, hivyo kupitia Mfumo huo ni wazi kwamba vijana wanaweza kuwa na hoja za msingi wanapo fuatilia maendeleo ya kiuchumi na hatua ambayo Tanzania imepiga ukilinganisha na nchi nyingine hususani za Afrika.Mtaalamu wa Masuala ya Mawasiliano, Bi. Christina Dimosso (katikati), akigawa machapisho yenye taarifa za uchumi na fedha kwa Bi. Aisha Said, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025, kushoto ni Bi. Hadija Saidi.

Aidha,ametoa rai kwa wananchi kutembelea Banda la Wizara ya Fedha katika maonesho hayo ili kupata taarifa za kina kuhusu mfumo huo.Wataalamu kutoka Idara na Vitengo vya Wizara ya Fedha wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa tayari kutoa elimu kwa umma kuhusu Sera, uchumi, fedha na programu zinazotolewa na Wizara kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha).

Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo (Nanenane) kwa mwaka 2025 yalizinduliwa rasmi Agosti 1, 2025 katika Viwanja vya Nanenane Nzuguni jijini Dodoma na Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yanatarajiwa kuhitimishwa Agosti 8, 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news