Miaka 10 ya mapinduzi ya fikra,naomba ridhaa tuijenge Rufiji ya ndoto yetu-Mchengerwa

NA JOHN JAYROS

MBUNGE anayetetea Jimbo la Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema,katika kipindi chote amekuwa mtumishi wa watu, mwanamapinduzi wa kweli anayejali maendeleo ya wananchi, hivyo amewaomba wajumbe wampe ridhaa ya kuwaongoza ili kuendelea kuleta maendeleo.
Kauli hiyo ameitoa leo kwenye mkutano wa kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kesho kwenye kura za maoni kuwa mgombea wa jimbo hilo kwa mara ya tatu mfulizo.

Mkutano huo umefanyika Ikwiriri na uliohudhuriwa na maelfu ya wajumbe na wananchi waliokuja kusikuliza sera za watia nia wanne wa jimbo hilo ikiwa ni pamoja na Mhe.Mchengerwa anayetetea jimbo lake.
Amesema, katika kipindi chake cha miaka 10 cha mapinduzi ya fikra na mageuzi makubwa ya maendeleo jimboni humo kumekuwa na mabadiliko kwenye kila sekta.

"Ndugu zangu katika safari hii sote tumejionea mapinduzi na mafanikio yaliyopatikana hivyo nawaombeni kwa kasi hii hii nipeni imani ili tuendelee kufanya maendeleo ya kweli ya jimbo letu."
Ameongeza kuwa miaka 10 ya kazi, uaminifu, na uongozi thabiti imetosha kuonyesha mwelekeo wa wapi kwa kwenda.
Baadhi ya sekta ambazo amezitaja kuwa na mabadiliko na maendeleo makubwa ni pamoja na ongezeko kubwa la miundombinu ya sekta za elimu na afya , barabara na madaraja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news