Mtendaji Mkuu wa WMA atembelea Maonesho ya Nanenane Dodoma

DODOMA-Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Bw. Alban Kihulla, leo Agosti 8, 2025 ametembelea Maonesho ya NaneNane kitaifa, uwanja wa Nzuguni jijini Dodoma.
Akiwa katika Banda la WMA, Afisa Mtendaji Mkuu amewapongeza watumishi wa Wakala kwa kazi nzuri ya kuelimisha umma ambayo wamekuwa wakiifanya tangu kuanza kwa Maonesho hayo.
Amewataka kuendelea kutoa elimu ya vipimo kwa jamii hata baada ya Maonesho ili wananchi waelewe ni kwa namna gani Serikali kupitia WMA inawalinda kwa kuhakikisha vipimo vinavyotumika katika sekta mbalimbali ni sahihi na vinatumika kwa usahihi.

"Tuendelee kutumia majukwaa mbalimbali kutoa elimu ya vipimo kwa wananchi ili waelewe haki yao ya kupata huduma kwa vipimo sahihi lakini pia na wajibu wao wa kuhakikisha wanatumia vipimo sahihi katika sekta mbalimbali. "
Kihulla ametembelea mabanda mengine mbalimbali likiwemo banda la Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Taasisi zake ili kujionea huduma zinazotolewa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news