Turejee katika Maktaba: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na wajasiriamali wadogo wadogo katika Soko la Kijangwani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 18 Novemba,2020 alipofanya ziara ya kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara hao.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi tangu aingie madarakani mwaka 2020 amekuwa na utaratibu wa kuyafikia makundi mbalimbali ya wananchi kote Unguja na Pemba, kusikiliza changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi na kuyafikia maendeleo yaliyotarajiwa kote Zanzibar. Na hii ndiyo siri ya uongozi unaoacha alama Zanzibar, Zanzibar ya sasa imepiga hatua kubwa katika sekta mbalimbali,neema zaidi zinakuja,tuendelee kumuunga mkono.
