DAR-Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt.Yamungu Kayandabila amekutana na kufanya mazungumzo na Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya FINCA, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Bi.Nasama Massinda, walipofanya ziara katika ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam leo Agosti 28,2025.
Mazungumzo hayo yamelenga kujadili mwenendo wa utendaji wa Benki ya FINCA, hatua za kuimarisha huduma za fedha, pamoja na nafasi ya taasisi hiyo kongwe nchini katika kuongeza upatikanaji wa huduma jumuishi za fedha kwa wananchi.
Dkt. Kayandabila amesisitiza dhamira ya Benki Kuu kuendelea kusimamia kwa karibu utendaji wa taasisi za fedha nchini ili kuhakikisha zinaendeshwa kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji,weledi na uthabiti wa kifedha.





