ARUSHA-Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limetunukiwa tuzo maalum ya ufanisi na Ofisi ya Msajili wa Hazina kutokana na mchango wake mkubwa katika kuboresha mapato, faida, ukwasi na rejesho la mtaji wa Serikali.
Tuzo hiyo imetolewa katika Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichofanyika jijini Arusha na kufunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango.Mbali na NHC, washindi wengine katika kundi la mashirika yanayofanya biashara ni Bohari ya Dawa (MSD) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Tuzo hizo zilitolewa kwa kuzingatia vigezo vya kiuendeshaji kama ukuaji wa mapato ya ndani, udhibiti wa matumizi, kuimarisha faida, kuboresha ukwasi, rejesho la uwekezaji pamoja na maboresho ya utoaji huduma kwa jamii.









