ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Agosti 13,2025 amemteua Dkt.Halima Wagao kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti ya Udhibiti wa Leseni za Biashara katika Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda.
Vilevile, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua ndugu Mussa Juma Abdalla kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Umwagiliaji katika Wizara ya Kilimo,Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo.

