DAR-Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameondoka Zanzibar na kuwasili jijini Dar es Salaam tayari kushiriki Uzinduzi wa Harambee ya Kitaifa ya kuchangia Kampeni za Chama Cha Mapinduzi, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Harambee hiyo itazinduliwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo inafanyika leo tarehe 12 Agosti, 2025 katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.





