DODOMA-Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Ramadhani Msangi ameipongeza, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati zinazosaidia sekta mbalimbali hususan usafiri wa anga. Ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la TMA katika maonesho ya NaneNane kitaifa katika Viwanja vya Nanenane Nzuguni jijini Dodoma.
Bw. Msangi amesema, pamoja na Mamlaka ya Usafiri wa Anga kuwa wadau wakubwa wa huduma za hali ya hewa, huduma hizo ni nguzo muhimu kwa sekta zote kwa vile shughuli nyingi zinaweza kuathiriwa na hali ya hewa.
Tags
Habari
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Tanzania Meteorological Agency (TMA)
TCAA Tanzania
Utabiri wa Hali ya Hewa Tanzania

