Utafiti wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) umebainisha uwepo wa mianya ya rushwa mipakani.
"Hela zimeisha, yaani shida hela zimeisha, umeelewa mzee? Mtu unakaa siku saba hapa, hela zimeisha,"anaeleza mmoja wa madereva ambao wanakumbana na adha ya foleni ya malori yanayosafirisha mizigo kuelekea mataifa mbalimbali eneo la Tunduma, ni foleni ambayo huwa inachukua siku tano hadi saba, na wakati mwingine zaidi.