Watakiwa kuendelea kuelimisha umma kuhusu shughuli za Ofisi ya Waziri Mkuu

DODOMA-Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena ametoa rai kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waendelee kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utendaji wa taasisi na programu mbalimbali zinazosimamiwa na ofisi hiyo.
Kauli hiyo ameitoa leo Agosti 2, 2025 alipotembelea banda la Ofisi hiyo akiwa ameambatanan na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dkt. Stephen Nindi na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri katika Maonesho ya Naneane yanayofanyika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
"Wananchi wanauhitaji kubwa wa kufahamu shughuli zinazoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, hivyo kuna umuhimu wa kuandaa vipindi vya kuelimisha umma,” alieleza.

Maonesho ya Wakulima maarufu Nanenane yamebebwa na kauli mbiu isemayo: "Chagua Viongozi Bora, kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025"

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news