ZANZIBAR-Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Riziki Pembe Juma amewataka Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Jeshi la Polisi kuendelea kuimarisha amani na usalama kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ili uchaguzi huo ufanyike katika hali ya utulivu.

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa elimu kwa Mtandao wa Polisi Wanawake pamoja na kuwaaga askari wa kike 27 wanaostaafu kazi kwa mujibu wa sheria, Mheshimiwa Pembe amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuanzisha na kuendeleza mtandao huo na amehimiza ushirikishwaji wa askari wa kike katika kazi mbalimbali za polisi ili kuleta usawa wa kijinsia.




