DODOMA-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza kuanza kwa awamu ya pili ya mazingira ya majaribio ya teknolojia ya fedha yanayodhibitiwa na benki hiyo.
Fursa hii inalenga kuchochea ubunifu katika sekta ya fedha huku ikihakikisha ulinzi wa watumiaji na uthabiti wa mfumo wa kifedha nchini.

